MWAFRIKA NA HOJA YANGU ; A Swahili Poem

Hivi Kipi Kati Ya Hivi Chenye Mamlaka?? Na Ni Kipi Chenye Nguvu??? JE NI NCHI MOJA MOJA KAMA BURUNDI AU NI OAU a.k.a AU??????????????? Kipi Kina Thamani Zaidi Ya Hivi???? Na Kipi Tunakithamini Zaidi???????JE NI UHAI WA MWAFRIKA MMOJA MMOJA AU WA WENGI????Kipi Tunakiepuka Hapa? NI MAUAJI TUNAYOYASHUHUDIA AU ZIMWI LA KIMBALI??(maana nasikia watu wakilizungumzia zimwi wakati mto kagera unajazwa mizoga ya watu kila siku) KIPI HASWA TUNATAKA KUONA NDIPO TUKUBALI MAMBO HAYA YALIPOFIKA SIO PAZURI. MPAKA LINI MAGHARIBI ITAZUNGUMZA KWA NIABA YETU, MAMBO YA KWETU ANGALI TUNATEMBEA VIFUA MBELE TUKIJIITA NCHI HURU?? MBONA YA KWAO WANAYASITIRI NA KUYANENEA VYUMBANI?   Nasikia Kelele Masikioni, Kila Nikiwasha NaKutega Sikio Redioni// Naona Vigelele Machoni, Sitambui Ni Shangwe Au Mikanyago Ya Majani Makavu Mafichoni// Ni Vipi Nitadumu Na Haya Moyoni// Na Vipi Nitazunguka Bila Haya Usoni// Mambo Haya Makuu Yapo Pomoni// Maneno Yamekubuu Mwangu Mdomoni// Nanena Nisiyoyaamini/ Natenda Kinyume Rohoni//  Nadhani Mazoea Binti Mito Mingi Ndio Upofu Sioni// Nakimbilia Wahisani Kuleta Suluhu Ya Moyoni// (Nacheka) Kwani Mikono Haitenda Jema Na Miguu Yaongeza Mwendo Upotevuni// (Napeta) Hakika Mbio Zangu Hazina Mwisho Zaidi Ya Kuishia Sakafuni// Na Hata Wakicheka Nitafurahi Kuona Furaha Ya Wakuu Ipo Pomoni// Maana Mama Aliniambia Nijaze Heshima Bila Kuwajali Wandani// Ikibidi Hata Kuwaua Na Njaa Hawa Nyumbani// Magonjwa Hata Vita Sitolaani// Vipi Nitadumu Na U-Kaksi Huu Jamani//  Mimi Ni EI-YU Na Nakupenda Sana Mwandani// Sema Nitampa Ufunguo Wa Chumbani// Huyu YU-ENI Amtendee Uzinzi Mwandani// Aje Na Washirika Ndivyo Apendavyo Mwandani// Kama PILATO Nitanawa Mikono Hii Hamu Ya Mwandani// Sina Haki Nayo JAMANI. N I S A M E H E MAANANI. Mbona Hata I-EI-SI Hana Mpango Jamani// Au Hamumuoni Akiteta Na Washirika Faraghani// Nisameheni Maana Nipo Kujifua Na Vyuma NAAHIDI NITAPIGANA MWAKANI// Naomba Muendelee Kufa KWA AMANI// Sina Ubabe Nami Ni Mtumwa Jamani//  #NikikosaUsingiziHuwaNazichoraKutaZaChumbani#Afrika

 

This poem is about: 
Our world
Poetry Terms Demonstrated: 

Comments

Need to talk?

If you ever need help or support, we trust CrisisTextline.org for people dealing with depression. Text HOME to 741741