Baa-Medi
Usiku mnene
Mwenyewe kwenye kichochoro
Tochi haina mawe- giza totoro
Mvua,Radi hadi malinzi washadoro
Hatari Mbwa Wakali Wamekata Minyororo
Chocho Ngalimi -Si chocho Ngarenaro
Utamwambia nini– sahiyo kumi kasoro
hutoka Kazini -na mfuko wa malboro
Hatari Mbwa wakali wamekata Minyororo
mezani Makombo-hukombeleza kama soro
mabaki ya nyama choma na makongoro
silaha ya baamedi kwenye vichochoro
hatari Mbwa wakali wamekata minyororo
we chukulia mzaha- amenizaa ni mzazi
kazini ni baa - we huenda baada ya kazi,
weekend balaa – ye hutingwa na kazi
Njaa-Hatari mbwa wakali wamekata minyororo
Usiku mmoja hupiga kazi ka msukule
mi humngoja- nimsimulie za shule
Hurudi mchovu na asiyetaka kelele
Shukrani-Mkono kinywani Daily
Usingizi baada ya simulizi ni njozi
Njozi ya ufumbuzi Utatu Utatuzi
Kazi ni Kazi- Kazini kwake ni Baa
Namuita Mama we muite Baamedi
-Matei Babu 2016