PoemsBrowse PoemsSlamsFresh DropEchoes
LearnWriting TipsPoetry TermsPoets & ArtistsBooksFor Teachers
ExplorePoetry GenomePoem MapEchoesTake ActionGroups
AboutWrite a PoemDonateSign UpLog In

HUNTER VIRUS NA CORONA


Hunter virus na Corona, Tumekuja kwa maana, Shetani si muungwana, Afanya yawe mapana, Msahau Maulana, Mpate zake laana, Wivu mkishikamana, Na mkisaidiana. Yu anafanya uhuni, Watu wako majumbani, Ataka wajaribuni, Msiende darasani, Msiende makazini, Uchumi uwe gizani, Ili mfeli shuleni, Mkate matumaini. Elimu ya Maanani, Wafata ya duniani, Ambayo ni ya mbinguni, Mtailudia lini? Rudini kwenye dini, Hebu hata shtukeni, Sie twawakumbusheni, Dunia iko mwishoni. Twapita tu njiani, Ili tuwatisheni, Tokeni dhambini, Rudini kwenye imani, Elimu i hadharani, Ipendeni moyoni, Dawa hio chukueni, Ya swala na Quran.
©All Rights Reserved

Something wrong with this poem?

Share

Replies are closed for this poem.

Husna Chikwela

A beutiful poeter from Tanzania. I write both english and swahili poems especially tradition poems

View all poems →

Your Poem's Voice

See what makes your poem unique — its voice, energy, themes, and the literary traditions it draws from.

Comments (0)

No comments yet. Be the first to share your thoughts.

Log in to leave a comment.